{"id":1625487,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625487/?format=json","text_counter":238,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ikiwa kuna wahuni wanaoingilia maandamano na kuleta vurugu, kuiba, kudhulumu na kuumiza wananchi, kuna mpangilio unaofaa kufuatwa wa kushikwa, wapelekwe kortini na kuhukumiwa kwa sababu sheria zetu zinasema mtu hana hatia mpaka ithibitishwe kortini."}