{"id":190314,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/190314/?format=json","text_counter":30,"type":"speech","speaker_name":"Ms. Leshomo","speaker_title":"","speaker":{"id":379,"legal_name":"Maison Leshoomo","slug":"maison-leshoomo"},"content":"Bw. Spika, nimeshtuka sana kusikia kwamba Waziri Msaidizi hana jibu ilhali watu wanakufa na mali yao kuibwa. Watoto wameacha shule. Hakuna mtoto aliye shuleni katika tarafa hizo zote. Pia watoto wanakufa. Tarehe 1 Julai, 2008, nililia machozi nilipopigiwa simu kwamba watu wanakufa. Je, Serikali ina mpango gani kusimamisha vita hivyo? Kwa wakati huu, kuna njaa huko. Watu wanakufa na ng'ombe wanaibwa. Je, tutaelekea wapi?"}