{"id":213864,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213864/?format=json","text_counter":58,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Mwandawiro","speaker_title":"","speaker":{"id":253,"legal_name":"Mwandawiro JD Mghanga","slug":"mwandawiro-mghanga"},"content":"Bw. Spika, tatizo la watu kujeruhiwa hata kuuawa na wanyama wa porini kama vile nyoka, ndovu, simba na fisi ni halisi na linaendelea sana, hasa katika Wilaya ya Taita-Taveta. Je, Wizara ina mipango gani halisi ya kuwafidia watu mara moja wakati wamekumbwa na tatizo kama hilo? Hesabu ya Kshs200,000 hazitoshi kumfidia binadamu ambaye amejeruhiwa na mnyama ama kuuawa?"}