{"id":214600,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/214600/?format=json","text_counter":69,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Mwandawiro","speaker_title":"","speaker":{"id":253,"legal_name":"Mwandawiro JD Mghanga","slug":"mwandawiro-mghanga"},"content":"Bw. Spika, ninashangaa! Huyu Waziri anatoka Mkoa wa Pwani na anaelewa sana kwamba katika mbuga ya wanyama pori ya Tsavo kuna wanyama pori wengi. Watu wa eneo kama Taita-Taveta hawafaidi chochote na huku kando nyama hii inauzwa katika mahoteli. Je tutaendelea kuwaambia watu wetu wachunge hizo kanga ili kutosheleza mahitaji ya mabepari wakati hawapati chochote?"}