{"id":261705,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/261705/?format=json","text_counter":94,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Hassan","speaker_title":"","speaker":{"id":398,"legal_name":"Yusuf Hassan Abdi","slug":"yusuf-hassan-abdi"},"content":"Asante, Bw. Spika. Waziri Msaidizi amesema Mawaziri wa Afrika Mashariki wamesikilizana kulishughulikia swala hili la kwekwe. Pengine angetunufaisha na kutuelimisha hapa katika Bunge, Mawaziri hawa wana bajeti ya shilingi ngapi? Na ni jinsi gani watashughulikia matatizo tuliyonayo kwenye ziwa letu hapa nchini Kenya?"}