{"id":277828,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277828/?format=json","text_counter":299,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Joho","speaker_title":"The Assistant Minister for Transport","speaker":{"id":30,"legal_name":"Hassan Ali Joho","slug":"hassan-joho"},"content":" Bi. Naibu Spika wa Muda, naona kuwa ndugu yangu hajajua jambo la nidhambu ni nini. Nimesema hivyo kwa sababu sina raha kuona mtu anasema ati sisi ni GEMA; sisi ni KAMATUSA; tunataka tusikie kuwa sisi ni Wakenya. Ninasema hivi, hata kwa wale ndugu zangu walioko Mombasa; nawaambia wasiseme kuwa Pwani si Kenya. Ningefurahi hata viongozi wa kutoka maeneo ya GEMA, KAMATUSA na kadhalika wakisema kwanza wao ni Wakenya. Kwa hivyo hiyo isikutishe; pengine Kiswahili chakuchanganya. Baadaye tukitoka pale nje, nitakuambia kwa Kimombo ili uelewe vizuri."}