{"id":315158,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315158/?format=json","text_counter":314,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Mwadeghu","speaker_title":"","speaker":{"id":98,"legal_name":"Thomas Ludindi Mwadeghu","slug":"thomas-mwadeghu"},"content":"Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaomba kuunga mkono Mswada huu. Watu wengi wameathirika kutokana na mpango huu ambao, wengi wetu tunauita “merry go-round”. Watu wengi wamestaafu, wakaweka hela zao katika mpango huu na wamepoteza fedha zao. Ninamshukuru mhe. Khalwale kwa kuuleta Msada huu na ninaomba sote tuunge mkono."}