{"id":3364,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/3364/?format=json","text_counter":209,"type":"speech","speaker_name":"Dr. Shaban","speaker_title":"","speaker":{"id":139,"legal_name":"Naomi Namsi Shaban","slug":"naomi-shaban"},"content":"Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumueleza Mbunge mwenzangu kwamba hawa watu wane, ambao hawako kwenye orodha, hawajawahi kulipwa hata mara moja; kwa sababu hiyo, watafikiriwa kuwekwa katika orodha ya walengwa wakati watu watakapokuwa wakiongezewa; kama watafaa kuwa kwenye orodha, basi wataorodheshwa. Kwa sasa, hawako kwenye orodha ya walengwa tuliyo nayo."}