{"id":359671,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/359671/?format=json","text_counter":135,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Bima tunayozungumzia inaweza kuleta matatizo baadaye, kwa sababu hakuna mwaka ambao ngâombe hawafi. Wakati wa nyuma kwetu Kinango ndiko kulikuwa na soko kubwa zaidi la kuuza wanyama na ngozi. Hivi sasa, watu wangu wanashangaa kusikia Mbunge aliyenitangulia kuongea akisema kwamba mashamba yetu yanakaa bure. Hatutaki yakae bure. Lakini ngâombe wetu wanakufa. Kwa hivyo, ningeomba awe na shukurani kwa sababu tumewaachia nafasi. Wakati tutakapopata pesa za kunyunyuzia maeneo yetu maji, wanyama wao hawatakuja kwetu kwa sababu tutakuwa na wanyama wa kutosha."}