{"id":371190,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/371190/?format=json","text_counter":255,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Huka","speaker_title":"","speaker":{"id":2240,"legal_name":"Mohamed Adan Huka","slug":"mohamed-adan-huka"},"content":"Asante kwa kunipatia nafasi hii Mhe. Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii si kwa sababu haya ni mambo mapya ambayo yameletwa. Kuna methali ambayo inasema: âBaniani mbaya kiatu chake dawa.â Hii inamaanisha kwamba hata kama Hoja hii imeletwa na CORD, ina faida kwa Jubilee kwa sababu Serikali ya Jubilee ni Serikali ya kusema na kutenda."}