{"id":413002,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/413002/?format=json","text_counter":754,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ningependa kuangazia Mswada huu kwa sababu kuna mbinu za kichini chini za kuhakikisha kwamba wale Mawaziri-Katibu wanajilimbikizia mamlaka ambayo hata Rais mwenyewe hana. Utakuta vipengele vingi ambavyo vinapendekezwa hapa vikisema kwamba Waziri-Katibu aweze kuwa na nafasi ya kuteua bila idhini ya Bunge hili la Kitaifa. Hilo si jambo la busara."}