{"id":415414,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/415414/?format=json","text_counter":269,"type":"speech","speaker_name":"Sen. (Dr.) Machage","speaker_title":"","speaker":{"id":179,"legal_name":"Wilfred Gisuka Machage","slug":"wilfred-machage"},"content":"Shukrani, Bw. Spika. Yale niliyo yasikia kutoka kwa viongozi wa Kamati tuliyoiunda ni kama hadithi za Alfu Lela U Lela. Mengine ni zaidi ya hekaya za abunuasi kwa sababu kuwapa wananchi mbegu za kupanda zisizo ota ni kama vile abunuasi alimulikiwa na mwanga wa tochi kwamba apate joto la baridi."}