{"id":442451,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442451/?format=json","text_counter":367,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Kila mahali sisi tunakoenda, tunahubiri amani. Kwa hivyo, haya mambo ya mapambano, guruneti na sijui nini; wananchi wanauliza, je huu ni wakati wa kupiga siasa au kufanya kazi? Wacha watupatie nafasi sisi, kama Serikali ya Jubilee, ili tufanye kazi; nao wangoje hadi mwaka wa 2017 ndipo watuambie tumefanya nini."}