{"id":445892,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/445892/?format=json","text_counter":105,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kombe","speaker_title":"","speaker":{"id":250,"legal_name":"Harrison Garama Kombe","slug":"harrison-kombe"},"content":"Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Swala la barabara si swala la Githunguri na Ruiru pekee. Tulipitisha Hoja hapa kuhusu kilomita 20 za barabara katika kila eneo-wakilishi la Bunge. Pengine Mwenyekiti angetuelezea ni lini mipango hiyo itaanza katika kila eneo-wakilishi la Bunge ili barabara zipitike vyema. Wizara ina mipango gani ili miradi hiyo ianze mara moja kwa sababu mwaka wa kwanza umepita na hakuna chochote kimeanza?"}