{"id":448227,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/448227/?format=json","text_counter":28,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Wario","speaker_title":"","speaker":{"id":252,"legal_name":"Ali Wario","slug":"ali-wario"},"content":"Mhe. Spika, ninaomba mwongozo kutoka kwako. Wakati Mbunge mpya anapolishwa kiapo cha ofisi tunalazimika kusimama. Kanuni za Bunge, Vipengele vya 3 na 104 havisemi kwamba ni lazima tusimame wakati Mbunge mpya anapolishwa kiapo. Mwongozi wa sisi kusimama wakati Mbunge mpya analishwa kiapo umetoka wapi? Naomba mwongozo kutoka kwa Mhe. Spika."}