{"id":474219,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/474219/?format=json","text_counter":122,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kombe","speaker_title":"","speaker":{"id":250,"legal_name":"Harrison Garama Kombe","slug":"harrison-kombe"},"content":"Mhe. Naibu Spika, niliuliza taarifa kutoka kwa Mwenyekiti anayesimamia Kamati kuhushu Ardhi. Hajakuwepo Bungeni kwa muda mrefu. Leo nimemuona. Ni matumaini yangu kwamba nitaweza kupata taarifa hiyo sasa hivi, maana alikuwa amenidokezea kwamba yuko tayari, na anangoja tu kuulizwa aitoe taarifa yake."}