{"id":474825,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/474825/?format=json","text_counter":42,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Wario","speaker_title":"","speaker":{"id":252,"legal_name":"Ali Wario","slug":"ali-wario"},"content":"Pili, makurutu waliambiwa wakimbie. Huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ikiwa hii ndio mbinu inatumika kujua kurutu bora na hali wengine walikuwa wamefunga; je walikimbia sawa na wale ambao hawakuwa wamefunga? Je, hii si ilikuwa dhulma kwa Waislamu?"}