{"id":507786,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/507786/?format=json","text_counter":245,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Mwadeghu","speaker_title":"","speaker":{"id":98,"legal_name":"Thomas Ludindi Mwadeghu","slug":"thomas-mwadeghu"},"content":"Mheshimiwa Spika, naomba nitoe mchango wangu kwa Ripoti hii ya Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma ambayo imechambua mambo mengi kuhusu uendeshaji wa mashirika mbali mbali ya nchi hii. Haswa, naomba nielekeze mwelekeo wangu kwa Shirika la Reli la Kenya ambalo lilichangia sana kuona kuwa kazi ya uendeshaji wa reli imepeanwa kampuni iliyokuwa mbichi, geni, mwanamwali na isiyoweza kufanya kazi. Kampuni hii ilikuwa inatoka Afrika Kusini na kazi yake haikuwa imetambulika au kueleweka vizuri. Hata hivyo Mheshimiwa Spika, ikabainika wazi kuwa Shirika la Reli la Kenya lilitakikana lipeane kazi hii kwa kampuni hiyo. Wakati mmoja ilibidi wakuu wa Serikali waje waone Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma ili waweze kujieleza kwa sababu Kamati hii ilikuwa imeomba tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi ichunguze kwa undani waliokuwa Mawaziri wa Usafirishaji na Fedha tangu hapo awali. Mawaziri hao walikuwa Mhe. Kimunya, Mhe. Chirau Ali Mwakwere na Mkuu wa Fedha Joseph Kinyua na Esther Koimett kwa sababu ya yale waliyotenda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."}