{"id":530826,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530826/?format=json","text_counter":113,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Mwaura","speaker_title":"","speaker":{"id":13129,"legal_name":"Isaac Maigua Mwaura","slug":"isaac-mwaura"},"content":"Mhe. Naibu Spika, kwa sababu naona muda wangu umeenda sana, mara nyingi twarejelea lugha yetu ya Kiswahili kwa sababu wahenga walisema kuwa “mwenda tesi na omo marejeo ni ngamani”. Kwa sababu muda hauniruhusu na Waswahili husema “ana maneno mengi kama chiriku aliye kunywa maji ya chooni”. Mimi sijayanywa na ninaunga mkono Hoja hii."}