{"id":566966,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566966/?format=json","text_counter":332,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"uwezo wa kuangalia maisha yangu; kwamba naweza kulala vizuri, kuamka vizuri na nikaja hapa. Sio kama wakati wa mwaka 2001, wakati wa mhe. Rais Moi, ilikuwa huwezi ukaua Mkenya bila kupatikana. Walikuwa wanachukua jukumu kwamba lazima maisha ya Mkenya yalindwe kwa vyovyote vile. Na hatukuona mtu yeyote akifa. Wakenya katika hii nchi wanatakikana kulindwa vilivyo. Tunasema tuko na shirika la uchunguzi la NIS. Wanachunguza nini ilhali Wakenya wanakufa? Kwa nini hao wakubwa wa uchunguzi walio katika mamlaka hawawezi kufanya kazi yao? Mhe. Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Kenya. Kwa nini mhe. Rais asiwafute kazi kama wameshindwa halafu awachukue vijana awaweke kwenye maofisi wafanye kazi? Mwisho, tusilinganisha dini na uharamia."}