{"id":575593,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575593/?format=json","text_counter":48,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Mwadime","speaker_title":"","speaker":{"id":2451,"legal_name":"Andrew Mwadime","slug":"andrew-mwadime"},"content":"Shukrani, Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono hili swala. Kwa kweli hawa wazee wa vijiji ni watu muhimu sana, manaake kawaida viongozi huwatumia hawa watu na baadaye wanawasahau. Ni vyema wangewaangalia kimfuko manaake wao kwa upande wa usalama ndio nguzo. Kila mtu anayeingia katika kijiji ndio wanaomfahamu. Ukiangalia maswala mengine kama kesi ndogo ndogo, wao ndio hutumika. Ni vyema tuwaangalie vizuri hawa wazee wa vijiji. Naunga mkono kwa dhati kabisa maswala ambayo wenzangu wamezungumzia."}