{"id":588066,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/588066/?format=json","text_counter":58,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Nilizungumza na rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa karibu sana na Rais Kibaki, kwamba nilikuwa naomba kuja kuona mmefikia wapi. Nilipofika, Rais Kibaki akaniambia mambo mawili; kwanza, nimwambie Kofi Annan asiondoke kwani wakati huo walikuwa wameshavunja mazungumzo. Na, aliyeniletea ujumbe huo ni Moses Wetangula."}