{"id":591270,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/591270/?format=json","text_counter":336,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Naibu Spika wa Muda, jambo lingine linalochangia kukosekana kwa nidhamu kwa wanafunzi, ni ile hali ya sisi kama wazazi kuwapa fedha zaidi. Wanafunzi wanatumia fedha hizo kwa njia moja au nyingine kuharibu maisha yao."}