{"id":595562,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595562/?format=json","text_counter":178,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mbuvi","speaker_title":"","speaker":{"id":80,"legal_name":"Gideon Mbuvi","slug":"gideon-mbuvi"},"content":"Asante, Bw. Spika. Nimerudi leo hapa Seneti baada ya kupotea kwa muda mrefu. Nilikuwa naomboleza marehemu baba yangu. Nachukuwa fursa hii kama Seneta wa Kaunti ya Nairobi kuwakaribisha ndugu zetu kutoka Kaunti za Kilifi na Vihiga. Karibuni sana Nairobi. Mjihisi nyumbani. Mimi ni mwenyeji wa Kaunti ya Kilifi kwa sababu nina boma huko. Nitaongea na Sen. Khaniri anitafutie boma nyingine katika Kaunti ya Vihiga ile tuzidishe upendo kama viongizi wa Jamuhuri ya Kenya. Karibuni sana na mjihisi nyumbani."}