{"id":620812,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620812/?format=json","text_counter":146,"type":"speech","speaker_name":"Hon. (Ms.) Khamisi","speaker_title":"","speaker":{"id":874,"legal_name":"Mishi Juma Khamisi","slug":"mishi-juma-khamisi"},"content":"Pia nataka kusema ya kwamba ndugu zetu wengi walemavu katika taifa hili la Kenya ni masikini. Umasikini huu umesababishwa na yale maumbile walio nayo. Wengi wameshindwa kwenda shule au kwenda kwa taasisi za masomo kwa sababu ya kukosa vifaa vinavyohusika kuweza kuwasomesha wapate taaluma. Hivyo basi wamekuwa wakiishi katika maisha ya uchochole."}