{"id":627571,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/627571/?format=json","text_counter":119,"type":"speech","speaker_name":"Hon. (Ms.) Lay","speaker_title":"","speaker":{"id":1022,"legal_name":"Joyce Wanjalah Lay","slug":"joyce-wanjalah-lay"},"content":"Ninashukuru sana Mhe. Spika kwa fursa hii ya kuweza kuchangia Mswada huu kuhusiana na shamba za jamii. Kama tujuavyo, shida hizi za mashamba zimetukumba haswa sisi wakazi wa Pwani, Taita Taveta ikiongoza. Ni vizuri tukiwa na Mswada ambao unaweza kuambatana na Katiba yetu ya mwaka 2010. Lakini vile vile pia, tutasubiri wakati ambao utafika wa kuweza kufanya marekebisho kwa sababu kunayo marekebisho mengi ambayo yanastahili kuongezwa kwa Mswada huu."}