{"id":640074,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640074/?format=json","text_counter":215,"type":"speech","speaker_name":"Hon. (Ms.) Khamisi","speaker_title":"","speaker":{"id":874,"legal_name":"Mishi Juma Khamisi","slug":"mishi-juma-khamisi"},"content":"Tatizo hili la maradhi haya limekuwa kwa sababu nchi yetu bado haijaweza kuwa na taasisi ama zahanati zinazoweza kupigana na maradhi hayo na kuweza kukimu wakenya wengi ambao wamepata hayo matatizo. Inabidi Wakenya wengi wasafiri kutoka sehemu mbali mbali za Kenya kwenda kwa hospitali yetu kuu ya Kenyatta ili waweze kupata matibabu, na zile huduma ambazo zinafanyiwa wagonjwa walio na saratani sampuli tofauti tofauti. Kuyatambua maradhi ya saratani imekuwa tatizo sugu kwa sababu madaktari wengi hawana taaluma ya kuyatatua. Hivyo basi, wagonwa wengi wanaotembea kwa hospitali ama zahanati zetu wanakumbana na utata. Kwa mfano, kwa akina mama, saratani ya matiti, mwanamke anaweza kupata jipu au uvimbe mdogo. Mara nyingi, anapokwenda kwenye hospitali zetu za kawaida, anaambiwa pengine in jipu au uvimbe wa kawaida. Baadaye muda mchache, inapatikana ya kwamba ilikuwa ni saratani wakati ambapo imeshaenea na kumletea madhara makubwa sana. Nataka nitoe mapendekezo machache ambayo yanaweza kutusaidia sisi kama Wakenya kupigana na janga hili la maradhi ya saratani. Kwanza kabisa, lazima Serikani ishirikiane na mashirika yasio ya kiserikali ambayo yanapigana na maradhi ya saratani. Kwa mfano, kuna hili shirika la wagonjwa mahututi la Hospitali ya Pwani. Shirika hilo linawachukua wagonjwa takribani 2,000 kila mwaka ambao wana matatizo ya saratani. Matatizo ya saratani si tiba peke yake. Wagonjwa wa saratani lazima wapate ushauri na huduma zingine ambazo ni tiba-kemikali na tiba-redio; chemotheraphy and"}