{"id":649533,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/649533/?format=json","text_counter":193,"type":"speech","speaker_name":"Hon. (Ms.) Chidzuga","speaker_title":"","speaker":{"id":751,"legal_name":"Zainab Kalekye Chidzuga","slug":"zainab-kalekye-chidzuga"},"content":"Twende katika Kaunti ya kwale. Hapo awali kulikuwa kusafi sana. Hivi sasa kila mahali kuna makaratasi na kinyesi. Wakati umefika Bunge la Taifa lisimame kindete kuokoa mazingira, afya na nchi yetu kwa jumla bila kujali ni nani; tusimame kwa umoja tuamue."}