{"id":675012,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675012/?format=json","text_counter":123,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Chea","speaker_title":"","speaker":{"id":1694,"legal_name":"Mwinga Gunga Chea","slug":"mwinga-gunga-chea"},"content":"Mhe. Naibu Spika wa Muda, itafika mahali wale wafanyikazi wa serikali za kaunti watakuwa wanapata hela na wale wengine wanafanyia Serikali ya kitaifa itakuwa hawapati hela. Kutakuwa na migongano katika kazi na bila shaka Serikali ya kitaifa itaandikisha hasara."}