{"id":675230,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675230/?format=json","text_counter":131,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":128,"legal_name":"Richard Momoima Onyonka","slug":"richard-onyonka"},"content":"Ningependa kumjibu Dadangu, Mheshimiwa Mbarire, kuwa ukimwita mwanamke “mama” ni kumtunukia heshima kubwa sana. Kwa hivyo, katika kutatua shida hii, ni kuhakikisha kuwa Wabunge wenzangu, kama mama Cecily Mbarire, wamefundishwa lugha ya Kiswahili ili lugha yao ijumuike na kuwa safi."}