{"id":685741,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/685741/?format=json","text_counter":374,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Gichigi","speaker_title":"","speaker":{"id":1909,"legal_name":"Samuel Kamunye Gichigi","slug":"samuel-kamunye-gichigi"},"content":"Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nachukua nafasi hii kuwapongeza washindi walioshindia Kenya katika michezo ya Olimpiki. Ningetaka kuomba Serikali ikague mambo yanayofanyika katika shule zetu. Nilipoandaa mkutano na walimu wanaosimamia michezo, niligundua kuwa hatuna vifaa vya michezo katika shule zetu. Hivyo basi, hatutaweza kupata dhahabu nyingi kutoka sehemu nyingi nchini. Kama Kamati ya Leba, tutachunguza yale yaliyofanyika kule Rio ili kuhakikisha kuwa hayatafanyika tena. Ni lazima tuhakikishe kuwa pesa zinazopatikana katika michezo ya bahati nasibu zitumike humu nchini ili kukuza michezo."}