{"id":686510,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/686510/?format=json","text_counter":256,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":128,"legal_name":"Richard Momoima Onyonka","slug":"richard-onyonka"},"content":"Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Mswada huu umekuja wakati muhimu sana kwa sababu utaleta maendeleo nchini. Vyuo Vikuu vyetu vyote vina shida. Hata wanafunzi wengine ambao huhitimu kutoka vyuo vyetu hawawezi kuandika ama kuongea kama watu ambao wamesoma. Ningependa kusihi Bunge hili kuhakikisha kwamba tumeleta sheria ambazo zitasawazisha na kuleta usawa katika masomo. Kwa upande wa uwajiri wa wakuu wa vyuo, lazima wawe watu ambao wamesomea kazi hiyo. Wawe na nidhamu na wafanye hivyo vyuo visifike. Masoma lazima yawe ya kuendeleza nchi yetu kwa sababu wanafunzi wengine wakihitumu, wanakosa kazi. Ukiangalia miungano ya wanafunzi, imeleta ukabila, ukiukaji wa sheria, ukosefu wa nidhamu na mambo mengine. Ingekuwa vizuri kama sheria ingeletwa ili kurekebisha shida hizo."}