{"id":686511,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/686511/?format=json","text_counter":257,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":128,"legal_name":"Richard Momoima Onyonka","slug":"richard-onyonka"},"content":"Waziri wa Elimu, Dkt. Matiang’i alisema atajarabu kuhakikisha amebadilisha na kuleta uongozi mwema vyuoni mwetu. Sheria za vyuo vikuu ambazo zimekuwa zikileta shida lazima tuzibadilishe. Ingekuwa vizuri kama sheria ingepitishwa ya kuhakikisha, kwa mfano, Chuo Kikuu cha Kisii kimejijenga na kujiendeleza kabla ya kufungua matawi kote nchini."}