{"id":713044,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/713044/?format=json","text_counter":26,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"magavana wanachangia kwa muungano wao wa Council of Governors . Hili ni jambo la kushangaza. Je, wanatoa wapi pesa hizo na ni za kazi gani? Magavana wanasema kwamba wanaziweka hizo hela kujitayarisha kwenda kortini kujitetea ilhali waliowachagua wanataabika. Nataka kusalimu amri na kusema ya kwamba Kenya inaangamia kwa sababu hakuna usalama wala msaada. Wale ambao wamekusanya mali kidogo wanaishi katika nyumba kubwa, wamejikinga kwa kutumia milango ya vyuma na mbwa. Narudia maneno ya J.M. Kariuki, kwamba kati ya watu milioni kumi, kuna watu milioni 40 ambao ni maskini. Kwa hivyo, sijui kama ni risasi ama nini itazuia wananchi kudai haki yao na kuwalazimisha viongozi waache kuiba. Nawashukuru wakaazi wa Nyamira. Tutajaribu tunavyoweza lakini najua hakutakuwa na jawabu la kuwasaidia."}