{"id":716504,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/716504/?format=json","text_counter":336,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Naunga mkono marekebisho katika Mswada huu. Nataka kutoa mfano wa uchaguzi uliopita katika nchini Marekani. Tulitazama katika runinga, tukasikia kwa redio na kusoma kwa mitandao ya kijamii vile Wamarekani walilalamika kuhusu upigaji wa kura. Kuna wale waliolalamika ya kwamba walipokuwa wanapigia Bi. Clinton kura kwa kuweka kidole, kura tatu zilienda kwa Bw. Donald Trump. Hayo ni mambo dhahiri ambayo yanafanyika. Tukubali au tukatae, Ukweli ni kwamba yanafanyika. Tuko hapa kuhakikisha kwamba hatutapatikana na mambo kama haya. Bw. Spika, hakuna chombo chochote kilichotengezwa na mwanadamu ambacho ni kamili, kiwe juu ya hewa au majini. Chochote kinachotengenezwa na mwanadamu huwa si kamili na ni lazima tujitayarishe. Je, kukiwa na kasoro tutatumia mbinu gani? Ndugu zetu katika upinzani wamekataa jambo hilo lakini ndani ya mioyo yao wanakubali. Mfano mzuri ni kwamba kuna baadhi ya watu nchini ambao wakiwa kwenye vilabu wanahakikisha kwamba wana glasi tatu na simu nne. Hayo mnayakubali kwa sababu simu moja isipofanya kazi, zile tatu zitawaokoa. Bw. Spika, tutayakataa haya yote lakini ukweli ni kwamba ni lazima tuwe na kitu kingine ambacho kitatusaidia wakati kutakapotokea matatizo. Kwa hayo machache naunga mkono. Msione haya kuupigia debe Mswada huu."}