{"id":736561,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/736561/?format=json","text_counter":194,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Nakara","speaker_title":"","speaker":{"id":2926,"legal_name":"John Lodepe Nakara","slug":"john-lodepe-nakara"},"content":"Mhe, Naibu Spika wa Muda, mimi najua Kiswahili sanifu. Ningependa kupongeza Mheshimiwa mwenzangu. Je, ni halali kwa Mheshimwa mwenzangu kusema ya kwamba yule aliyekua upande wa Jubilee kuruka upande mwingine hastahili kushutumu mabaya yanayotendeka katika nchi? Ni lazima ninyamaze wakati ambao watu wangu kule Turkana wanakufa njaa ama hawapati chochote? Hata kama niko Jubilee lazima nishutumu maana Serikali iliyoko sasa ni ya Uhuru Kenyatta na yeye ndiye anashikilia uongozi na siyo Raila. Makosa yote yanaenda kwa yule anayeongoza."}