{"id":737659,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737659/?format=json","text_counter":166,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kipyegon","speaker_title":"","speaker":{"id":1453,"legal_name":"Johana Ngeno Kipyegon","slug":"johana-ngeno-kipyegon"},"content":"Ahsante sana Naibu Spika wa Muda. Kwa Bunge lijalo, sisi ambao Mwenyezi Mungu ataturuhusu turudi hapa tutahakikisha ya kwamba wale ambao watakaa kwa Kamati ya Implementation watahakikishe kwamba hii maneno imefuatiliwa mpaka mwisho. Baada ya kila miezi sita, tutaleta Hoja kuuliza ile mambo ya NYS yamefika wapi. Hii kashfa ya NYS hatuwezi kuiachilia kama ile ya Goldenberg. Tutaifuatilia mpaka tuhakikishe ya kwamba wale ambao walihusika wamechukuliwa hatua inayofaa kisheria. Naunga mkono."}