{"id":756008,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756008/?format=json","text_counter":57,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Mohamed Ali","speaker_title":"The Member for Nyali","speaker":{"id":13398,"legal_name":"Amin Deddy Mohamed Ali","slug":"amin-deddy-mohamed-ali"},"content":"Mhe. Naibu wa Spika, licha ya Hoja zote zilizotajwa majuzi na Rais – Hoja za Kenya na Ukenya ndani yetu – ningelipenda pia kuchukua fursa hii kuomba Bunge hili, chini ya uangalizi wako, katika siku za usoni kuwa makini na kutunga sheria kali dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya."}