{"id":756619,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756619/?format=json","text_counter":143,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ahsante Mhe. Spika. Ningependa kuchukua fursa hii, kwa niaba ya watu wa Kipkelion Mashariki kukushukuru na Naibu wako kwa kuchaguliwa tena kuwa Spika wa Bunge la Kitaifa. Ningependa pia kuchukua fursa hii kushukuru watu wa Kipkelion Mashariki kwa kunipa nafasi tena kuendelea kuwa Mbunge wao. Nitawatumikia kwa nguvu zangu zote nilivyowaahidi."}