{"id":758733,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758733/?format=json","text_counter":371,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Tuwei","speaker_title":"","speaker":{"id":13436,"legal_name":"Vincent Kipkurui Tuwei","slug":"vincent-kipkurui-tuwei"},"content":"Asante sana, Naibu Spika kwa kunipa fursa hii nichangie Hoja hili ambayo inatushangaza kwamba tarehe 22.9.2017, watu 10 walipoteza maisha yao kwa kioja ambacho hakieleweki. Ni jambo la kushangaza kwamba kwa karne hili, sisi wote tulioko hapa kama Wakenya tunaona maisha ya binadamu yakipotezwa ovyo ovyo. Tumepoteza familia hizi kwa sababu ya kuawa kwa mfanyibiashara mmoja. Hili ni jambo la kutushangaza wote kama taifa. Kama mtu mmoja amefanya uhalifu kwa kumuua mfanyibiashara, itakuwaje jambo la kijamii? Ni jambo la kushangaza nilipowasikia Waheshimiwa wa Emurua Dikirr na Kilgoris wakiongea. Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba sisi wote tukiwa viongozi na wafanyikazi wa Serikali lazima tuajibike. Jambo kama hili haliwezi kuchukuliwa kimzaha hivi. Watoto wamebaki yatima, wamama wajane na mwenye biashara amepoteza mali yake na kiini na sababu ya haya yote ni uhalifu. Je, sisi kama Wakenya, Wakristo na jamii inayoishi sehemu hiyo, jukumu letu ni nini katika hali ya kudumisha amani na sheria? Tunaambia pole Wabunge wa Emurua Dikirr na Kilgoris. Sisi kama viongozi lazima tuone ni sababu gani hali hiyo imetokea na tunaomba mtusaidie kabisa. Ninachukua nafasi hii kuwaomba wananchi wote wa Transmara, ambapo mimi hupitia kila mara na nimetembea pale kwa minajili ya harambee za kuchangia maendeleo ya nchi hii, wadumishe amani. Niliwapata wakiishi kwa amani. Tangu jadi, hata kimila, mavazi na matendo yao yanafanana. Ningewaomba kwamba jambo likifanyika wawachie vyombo vya usalama vifanye kazi ili watekeleze wajibu wao. Ningewaomba wasichukulie sheria mikononi mwao. Hasara ambayo tumepata kwa kitendo cha uhalifu imechukua maisha ya watu 10. Tunasema pole sana na ninachukua nafasi hii kwa niamba ya wananchi wa Mosop kusema pole. Pia, ninatoa rambirambi zangu kwa familia zote ambazo zimepoteza jamii zao. Tutaungana na jamii hizi kesho kwa maombi ya wafu ili tupate kuwaambia wananchi kwamba amani ni muhimu kuliko chochote. Mwisho, vyombo vya usalama viko katika kila kijiji. Silaha ziko miongoni mwetu. Silaha iliyotumika kumuua mfanyabiashara huyo ilikuwa bunduki. Je, tutaishi vipi kama bunduki The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."}