{"id":763204,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763204/?format=json","text_counter":130,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Ruweida Mohamed Obo","speaker_title":"The Woman Representative for Lamu County","speaker":{"id":786,"legal_name":"Ruweida Mohamed Obo","slug":"ruweida-mohamed-obo"},"content":"Pia kuna tatizo la kutokuwa na usalama ambalo linaletwa na wafugaji. Tatizo kubwa lililoko Lamu ni la ukosefu wa usalama ambalo limeletwa na Al Shabaab . Tulitoa suluhisho kwa kusema misitu iliyoko kando ya barabara ikatwe kwa kimo cha kilomita moja kila upande ndiyo wahalifu wakivamia watu waweze kuonekana virahisi."}