{"id":763762,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763762/?format=json","text_counter":55,"type":"speech","speaker_name":"November 7, 2017 SENATE DEBATES 11 Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa natuma risala zangu za rambirambi, za familia yangu na watu wa Laikipia kwa watu wa Nyeri kwa kumpoteza Gavana wao. Nilimjua kwa sababu ni jirani wetu. Alikuwa amejitolea mhanga. Kwanza, alikuwa amesema angeunganisha Kaunti ya Nyeri kwa sababu ilikuwa na mgawanyiko. Alikuwa ameweza jambo hili kwa sababu kwa muda ule alikuwa Gavana, nilizungumza na watu wa Nyeri. Walisema kuwa ni mtu aliyefanya vizuri. Anatambulika pia nchini kwa sababu alichangia sana wakati wa kutengeneza"}