{"id":7643,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/7643/?format=json","text_counter":306,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Ethuro","speaker_title":"","speaker":{"id":158,"legal_name":"Ekwee David Ethuro","slug":"ekwee-ethuro"},"content":"Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Waziri kwa Kiswahili sanifu. Waziri amesema kuwa barabara kutoka Kachibora hadi Sibanga inaelekea Kitale. Ningependa kumkumbusha Waziri kwamba, - inafaa ajue - barabara kutoka Kachibora mpaka Sibanga inapitia Makutano, Kapenguria mpaka Lodwar. Kwa vile amesema atatengeneza barabara hizo zote, je, atarekebisha lini barabara ya Sibanga- Makutano-Kapenguria-Lodwar? Ametenga pesa ngapi za kurekebisha barabara hii ili nami nimwalike Rais aje aifungue barabara hiyo?"}