{"id":7661,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/7661/?format=json","text_counter":324,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Ruto","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Hoja ya nidhambu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Bw. “Sonko” alisema kwamba kuna wanakandarasi fulani ambao wanatoa pesa; wengine pesa nyingi na wengine wanatoa pesa ndogo ndogo na akaendelea kueleza hao ni akina nani. Lakini sijui kama Waziri alikubali kama kuna wanakandarasi wa aina hiyo. Hakujibu swali hilo."}