{"id":776016,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776016/?format=json","text_counter":275,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Ali Sharif","speaker_title":"","speaker":{"id":2100,"legal_name":"Shariff Athman Ali","slug":"shariff-athman-ali"},"content":"Nikizungumza kwamba kuna nyumba imepigwa alama ya “X” na kuvunjwa, haijavunjwa, wala hakuna ilani yoyote. Ninataka kuhakikishia watu wa Lamu Mashariki wasiwe na hofu yoyote . Hakuna nyumba inavunjwa na Serikali iko pamoja na wao. Sidhani kama kutakuwa na maswala kama hayo. Maendeleo yapo na tumeyaona."}