{"id":806040,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806040/?format=json","text_counter":103,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Boy","speaker_title":"","speaker":{"id":13200,"legal_name":"Issa Juma Boy","slug":"issa-juma-boy"},"content":"Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Alikuwa ni Seneta mwenzetu ambaye nilionana naye wakati tulipokuwa tukiapishwa humu ndani na tukawa tumekaribiana sana. Lakini kama inavyosemwa, Mwenyezi Mungu ndiye mwenye uwezo. Mwenzetu alipigana na haya maradhi ya cancer sana, lakini Mwenyezi Mungu naye pia alichukua kiumbe chake kwa wakati huo. Kwa hivyo, kwa niaba yangu, niaba ya familia yangu na watu wa kaunti ya Kwale, natuma risala za rambirambi kwa familia ya Bw. Seneta mwenda zake, Sen. Okello."}