{"id":85216,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/85216/?format=json","text_counter":207,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Kutuny","speaker_title":"","speaker":{"id":61,"legal_name":"Joshua Serem Kutuny","slug":"joshua-kutuny"},"content":"Bw. Naibu Spika wa Mda, inasikitisha sana kwamba wakulima wamepewa kisogo na Serikali. Kwa sasa, wakulima wanafanya kilimo-biashara â siyo kilimo cha kuzalisha chakula peke yake â lakini inasikitisha kwamba Serikali imepunguza bei ya mahindi kutoka Kshs2,500 kwa gunia la kilo 90 mwaka uliopita mpaka Kshs1,500 hivi sasa. Waziri Msaidizi, afua ni mbili: Utangaze kwamba mtaongeza bei ifike Kshs2,500 kwa gunia ama ninakupatia ilani kwamba sisi, kama Wabunge, tutaitisha maandamano ya wakulima katika taifa la Kenya; watasusia kupeana mahindi yao kwa Serikali. Tayari Serikali imetangaza kwamba mwako ujao kutakuwa na---"}