{"id":893629,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/893629/?format=json","text_counter":21,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Asante sana Bw. Spika kwa kunikinga. Niliongea na vijana hawa na nikawaambia kwamba wakitia bidii katika masomo yao, chochote ambacho wanachotaka kuwa; wahandisi, marubani au mapadri, yote yawezekana. Ninawatakia kila la heri na wapeleke salamu zetu za Seneti kokote watakapoenda."}