{"id":908992,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/908992/?format=json","text_counter":170,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Bi. Spika wa Muda, Wakenya wengine wenye dini ya Kiislamu huambiwa kwamba lazima wafanyiwe vetting . Hakuna sheria inayosema kwamba lazima mtu afanyiwe vetting ndipo aweze kupata pasipoti. Ikiwa mtu ana kitambulisho au cheti cha kuzaliwa, hafai kufanyiwa vetting anapotafuta paspoti."}