{"id":922401,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922401/?format=json","text_counter":67,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Nataka kusema amefanya vizuri lakini kusema “ikiwa kuna dhuluma”--- Anapaswa kutohoa jina “dhulma” vizuri ndio liweze kueleweka na wale wote ambao wanaelewa ile lugha. Itakuwa ni jambo la kuwakejeli wanaoelewa hiyo lugha kwa sababu tutadhania ya kwamba maneno anayosema--- Mimi naonelea akiongea kwa lugha ya kingereza, huwa anajadili vilivyo kwa ufasaha na weledi. Lakini akiongea kwa lugha ya Kiswahili, inamkanganya kidogo mpaka hatumwelewi kabisa. Asante, Bw. Spika."}